RASMI : MAVUGO ATUA SIMBA AKABIDHIWA JEZI NAMBA 45

Mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi aliyekua akiichezea Vital O ya Burundi Laudit Mavugo ametua tayari Dar es Salaam kujiunga na wekundu wa Msimbazi Simba.


Mavugo amewasili Dar saa 4 usiku jana na kupokelewa na makamu Rais wa Simba Godfrey Nyange Kaburu na kukabidhiwa jezi namba 45.

Swala la Mavugo limechukua muda mrefu baada ya minong'ono kama pengine mchezaji huyo asingekuja nchini lakini sasa ni rasmi ametua na atatambulishwa katika Simba Day Jumatatu.

No comments

Powered by Blogger.