RASMI : MAN CITY YAMSAJILI JOHN STONES KWA PAUNDI MILIONI 50

Masaa machache baada ya Manchester United kutangaza kymsajili Paul Pogba kwa paundi milioni 100 majirani zao Man City nao wamemalizana na beki John Stones.


Stones anasajiliwa kwa dau la paundi milioni 50 ambalo Everton walikua wakitaka toka mwanzo

Stones mwenye miaka 22 anajiunga na Man City kwa mkataba wa miaka 6 akiungana na mageuzi makubwa ya Pep Guadiola ndani ya Etihad.

Tayari Man City walishaliweka jina la beki huyo chipukizi wa England katika kikosi chake kitakachoshiriki katika michuano ya ligi ya mabingwa hata kabla hawajamalizana na Everton.

No comments

Powered by Blogger.