NASRI,MANGALA NA WILFRIED BONNY WAONYESHEWA MLANGO WA KUTOKEA MAN CITY

Panga limewapitia wachezaji watatu katika kikosi cha Manchester City na kufungua milango kwa klabu zinazowataka kuwasajili kwaajili ya msimu ujao.


Beki aliyenunuliwa kwa pesa nyingi Eliquam Mangala,kiungo wa zamani wa Arsenal na timu ya taifa ya Ufaransa Samir Nasri na Wilfried Bony ni majina makubwa yaliyoachwa na klabu hiyo katika orodha ya wachezaji waliopelekwa majina yao UEFA kwaajili ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Manchester City chini ya Pep Guadiola itaanza kampeni yake kwa kucheza mechi ya mtoano dhidi ya Steau Bucharest wiki ijayo.

Katika orodha hiyo yumo pia beki John Stones ambaye jina lake lilipelekwa kabla ya kutangazwa rasmi kama mchezaji wa Man City toka Everton.

ORODHA KAMILI YA KIKOSI CHA MAN CITY KATIKA UCL

Makipa:
Joe Hart, Willy Caballero.

Mabeki:
Bacary Sagna, Pablo Zabaleta, Aleksandar Kolarov, Gael Clichy, John Stones, Jason Denayer, Nicolas Otamendi

Viungo:
Fernando, Raheem Sterling, Jesus Navas, Kevin De Bruyne, Fabian Delph, Leroy Sane, David Silva, Fernandinho, Yaya Toure.

Washambuliaji:
Nolito, Sergio Aguero, Kelechi Ihenacho


No comments

Powered by Blogger.