UEFA SUPER CUP : REAL MADRID KUIKABILI SEVILLA LEO BILA MASTAA KIBAO

Pambano la Uefa Super Cup kati ya bingwa wa michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya na bingwa wa michuano ya Europa league linapigwa leo usiku huko Norway.


Pambano hilo litazikutanisha timu mbili bingwa wa msimu uliopita zote zikitoka katika ligi kuu nchini Spain Real Madrid ambao ni mabingwa wa ligi ya mabingwa barani Ulaya na Sevilla ambao ni mabingwa wa Europa League.

Kuelekea katika pambano hilo Real Madrid itawakosa nyota wake kadhaa akiwemo mfungaji bora wa kihistoria wa michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya Cristiano Ronaldo pia itawakosa Mlinzi Pepe,kiungo Toni Kroos na mshambuliaji Gareth Bale ambao ni majeruhi na wamekosa mazoezi.

Mechi hiyo ambayo ni ya pili katika miaka mitatu baina ya timu hizo mbili katika Uefa Super Cup itaanza majira ya saa 4 kasorobo kwa saa za hapa Tanzania na ni mechi ya 3 mfululizo kwa Sevilla ambao wamekua mabingwa mara 3 mfululizo wa Europa League.


No comments

Powered by Blogger.