RAIS WA SIMBA EVANS AVEVA MIKONONI MWA POLISI KISA "PESA ZA OKWI"

Kamanda wa polisi Mkoa wa kipolisi Kinondoni, ACP Chistopher Fuime amethibitisha kumshikilia rais wa klabu ya Simba, Evance Aveva huku akishindwa kuweka wazi ni tuhuma gani zinazomkabili kiongozi huyo. wekundu wa Msimbazi alisema ni vizuri swali hilo.


"Tumemshikilia toka juzi jioni na juhudi za kupatiwa dhamana zimeshindikana mpaka dakika hii kwani sisi kazi yetu ni kumshikilia tu ila mamlaka zaidi yapo TAKUKURU."

"Kwa upande wangu siwezi kujua (Tuhuma zinazomkabili) ila kwa maelezo zaidi TAKUKURU wanaweza wakajua na ni lini huo uchunguzi utakamilika na kumpeleka mahakamani."

"Sisi tunamshikilia kwasababu TAKUKURU hawana mahabusu binafsi, na maswali yote wangejibu sababu hasa ya kushikiliwa kwa Evance Aveva."

Aveva anashikiliwa na polisi kwa kibali cha Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU lakini bado haijafahamika moja kwa moja anakabiliwa na tuhuma gani huku baadhi ya watu wakidai ni matumizi mabaya ya fedha walizolipwa kutoka Etoile Du Sahel juu ya malipo ya Emanuel Okwi pamoja na za Mbwana Samatta ambazo anadaiwa kuzihamisha kutoka kwenye akaunti ya klabu ya Simba.

Kwa upande wa TAKUKURU kupitia afisa habari Musa Misalaba amesema kuwa Aveva yupo kwenye mikono salama na wanamshikilia kwa uchunguzi,

"Kwa sasa wanaendelea na uchunguzi kwani sheria inaturuhusu kufanya uchunguzi na pia tunaruhusiwa kukamata, kupekuwa kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu."

No comments

Powered by Blogger.