KANTE AANZA KAZI CHELSEA IKIIKANDAMIZA AC MILAN BAO 3-1

Kiungo mpya wa Chelsea Mfaransa N'golo Kante ameanza kazi rasmi katika kikosi cha timu hiyo wakati Chelsea ikiibuka na ushindi wa bao 3-1 dhidi ya AC Milan.



Kiungo wa timu hiyo Oscar alifunga mabao mawili huku chipukizi Bertrand Traore akifunga bao moja kukamilisha ushindi kwa Chelsea katika mechi yake ya mwisho nchini Marekani.

Katika mchezo huo pia ulishuhudia mshambuliaji Diego Costa akirejea dimbani baada ya kuwa majeruhi na kuongeza nafasi ya machaguo katika safu ya ushambuliaji.

No comments

Powered by Blogger.