AHMED MUSA APIGA BAO 2 LEICESTER CITY IKIPOTEZA DHIDI YA BARCELONA

Mshambuliaji mpya wa Leicester City Mnigeria Ahmed Musa jana alifunga magoli mawili wakati Leicester City ikifungwa bao 4-2 na Barcelona.



Leicester City ambayo imetoka kukumbana na kipigo cha bao 4 pia siku chache zilizopita toka kwa PSG ilijikuta ikishindwa kufurukuta kwa mara nyingine katika mikono ya Barcelona.

Chipukizi wa Barcelona Munir alifunga bao 2 huku Suarez na Rafa Mujica wakifunga bao moja kila mmoja huku Ahmed Musa akifungua ukurasa wa mabao ndani ya Leicester City akifunga mabao hayo dakika ya 48 na 66.


No comments

Powered by Blogger.