JEZI ZA SIMBA NA YANGA KWA MSIMU MPYA ZAWEKWA HADHARANI

Wiki chache kabla ya kuanza msimu mpya wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara wadhamini wa ligi hiyo kampuni ya Vodacom Tanzania imetoa vifaa kwaajili ya timu zote zitakazoshiriki ligi hiyo msimu wa 2016/2017



Tayari Simba walishaweka wazi jezi zao mpya watakazotumia msimu wa 2016/2017 kabla ya kuonyeshwa rasmi leo ambazo zitaanza kuuzwa Simba Day zikiwa ni tofauti na za msimu uliopita.
Jezi za Simba
Kwa upande wa mabingwa wa Tanzania bara Yanga wao jezi zao zimeonekana pia kuwa na mwonekano tofauti na zile za msimu uliopita.
Jezi za Yanga 
Sambamba na jezi Vodacom imetoa vifaa mbalimbali kwa timu hizo ikiwa ni moja ya kipengele katika mkataba wake wa kuidhamini Ligi kuu Tanzania bara.




No comments

Powered by Blogger.