MAMBO YAZIDI KUMNYOKEA SAMATTA, GENK YATINGA HATUA YA MWISHO MTOANO UEROPA LEAGUE

Akicheza kwa dakika 77 mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayeichezea Genk ya Ubelgiji wamefanikiwa kutinga hatua ya mwisho ya mtoano katika michuano ya Europa League.


Genk ikicheza ugenini iliweza kuifunga Cork City  ya Jamhuri ya Ireland bao 2-1 katika mchezo wa marudiano hatua ya tatu ya mtoano .

Genk ilipata mabao yake kupitia kwa kiungo Thomas Buffel dakika ya 13 na Mlinzi Sebastien Dewaest dakika  ya 41

Ushindi huu unakamilishwa na ushindi wa bao 1-0 walioupata Genk katika mechi ya awali wiki iliyopita

Genk sasa imebakiza hatua ya mwisho ya mtoano kabla ya kutinga katika Makundi ambako timu kama Manchester United zitashiriki.


No comments

Powered by Blogger.