MOYES AANZA NA USAJILI WA BEKI TOKA CHELSEA

Kocha mpya wa Sunderland David Moyes ameanza rasmi usajili kwa ajili ya kuimarisha kikosi chake kwa kumsajili beki toka Chelsea Papy Djilobodji.


Beki huyo mwenye miaka 27 anajiunga na Sunderland kwa kiasi cha paundi milioni 8 na kufanya kuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na kocha huyo wa zamani wa Everton na Manchester United

Chelsea ilimsajili mchezaji huyo raia wa Senegal kutoka Nantes kwa paundi milioni 2.2 miezi 12 iliyopita.

Wakati huo huo Sunderland jana ilitoka sare ya bao 1-1 na Borussia Dortmund ya Ujerumani




No comments

Powered by Blogger.