JUVENTUS YAITAMBIA WEST HAM, CHELSEA YAIKANDAMIZA BREMEN

Mabingwa wa Italia Juventus wameifunga West Ham ya England bao 3-2 katika mchezo wa kirafiki uliopigwa katika dimba la Olimpiki Jijini London.


Juventus walitangulia kujipatia magoli mawili yakifungwa na Paulo Dyabala na Mario Mandzukic kabla ya Andy Caroll hajasawazisha bao zote hizo mbili huku goli la ushindi la Juventus likifungwa na Simon Zaza.

Katika mchezo mwingine wa kujiandaa na msimu mpya Chelsea imeifunga Werder Bremen ya Ujerumani kwa bao 4-2

Magoli ya Chelsea yamefungwa na Oscar,Hazard, Diego Costa na Pedro huku magoli ya Bremen yakifungwa na Claudio Pizaro na Lennart Thy.

No comments

Powered by Blogger.