KIPYENGA KINAPULIZWA HUKO WEMBLEY, HAYA UNAPASWA KUYAJUA UKITAZAMA MCHEZO WA NGAO YA JAMII KATI YA MAN UTD NA LEICESTER.

Na Richard Leonce

Huu ni mchezo wa 94 tangu michezo hii ya ngao ya jamii ianzishwe. Ni mchezo unaomhusisha bingwa wa msimu uliopita wa ligi kuu ya soka nchini England ambaye ni Leicester City, dhidi ya Manchester United mabingwa wa kombe la FA.

Ni mchezo wa 30 kwa Man UTD wakiwa wamefanikiwa kutwaa ngao hiyo mara 20 huku wakitwaa mara 5 kati ya 6 walizocheza mfululizo kuanzia msimu wa 2007/08 hadi 2013/14.

VIKOSI:
Leicester chini ya Claudio Ranieri watakua na mabadiliko kadhaa kwenye kikosi chao kilichocheza dhidi ya Barcelona. Golikipa Kasper Schmeichel anarudi langoni, huku Christian Fuchs na Shinji Okazaki wakichukua pia nafasi zao kutoka kwa Ben Chilwel na Demarai Gray.

Kwa upande wa Man UTD baada ya Ander Herrera na Morgan Schneiderling kucheza eneo katikati katika mchezo dhidi ya Galatasaray, leo watawapisha Michael Carrick na Marouane Fellaini. Jesse Lingard anaanza mahali alipoanza Henrikh Mkitaryan.

Man Utd: De Gea, Valencia, Bailly, Blind, Shaw, Carrick, Fellaini, Lingard, Rooney, Martial, Ibrahimovic.

Leicester: Schmeicher, Simpson, Huth, Morgan, Fuchs, Mahrez, Drinkwater, King, Albrighton, Okazaki, Vardy

No comments

Powered by Blogger.