WAINGEREZA KUTOKA WACHEZAJI BORA HADI REFA BORA.

Uhalisia wa maisha ni mabadiliko ya kila siku kwa mwanadamu lakini maisha haya yamebadilika vibaya kwa Waingereza ambao wanasifika kwa kuwa na mbwembwe,kupamba na kusifia vilivyo bora kutoka kwao.



Uhalisia huu umekuja katika kipindi ambacho Waingereza wamepoteza thamani ya kuwa na wachezaji bora wazawa katika ligi kuu na hata timu ya taifa ya Simba watatu hao.

Maisha ambayo wameyachagua yametuletea mtu tofauti kabisa kutoka kwa wachezaji hadi kutuletea mwamuzi bora wa dunia kwa sasa. Kamera nyingi za Waingereza zipo kwa Mark Clatternburg sasa ambaye amekuwa akichaguliwa kuchezesha fainali tatu katika msimu mmoja.

Si jambo jema sana kuwachimba kiasi hiki lakini kwa sasa Waingereza wamekosa wachezaji bora ambao ni icon yao katika ligi na hata timu ya taifa. Kizazi cha wakina Owen,Lampard,Rooney,Gerrard na wengine wengi kimepotea bila kuwa na mbadala sawia wa kuchukua nafasi za hao watu.

Ni Rooney pekee ambaye amekuwa akishindana na wengine nje ya nyumbani kwao kuanzia mikataba binafsi na hata mshahara katika timu. Uwezo wake umepulizwa na upepo kama mshumaa,Rooney wa sasa anaenda kumaliza mpira wake lakin hadi sasa hakuna wa kuvaa viatu vyake.

Clatternburg amekuja kuwa futa machozi Waingereza amekuwa kwenye ubora wa juu mno kipindi hiki na kuwasahaulisha machungu ya kutolewa katika mzunguko wa pili katika mashindano ya EURO2016 Ufaransa. Ndani ya msimu wa 2015-16 ameamua mapambano 3 makubwa. Amechezesha fainali ya FA,UEFA Champions League na UEFA Euro iliyopigwa Ufaransa.

Si fainali pekee amekuwa akitoa maamuzi yake hata mechi zile kubwa zilizo chini ya UEFA na FA amekuwa akipewa. Ubora wa Waingereza umepotea miguu na kuhamia kwenye filimbi. Safari yao imebadilika ghafla mno. Tusubiri kuona nani atawasahaulisha kuhusu Clatternburg na Gareth Bale ambaye ni mwanachama wao wa muunganiko wa nchi!!.

Imeandaliwa na Ayoub Hinjo 

No comments

Powered by Blogger.