TOTTENHAM YAMSAJILI BONGE LA MSHAMBULIAJI TOKA UHOLANZI

Klabu ya Tottenham Hotspur ya England imekamilisha usajili wa mshambuliaji Vincent Janssen kwa paundi milioni 18.5.


Janssen ambaye ni mshambuliaji wa kimataifa wa Uholanzi amesajiliwa na Tottenham Hotspur toka katika klabu ya AZ Alkmaar ya Uholanzi.

Mshambuliaji huyo mwenye miaka 22 amefanikiwa katika vipimo vya afya jana amesaini mkataba wa miaka minne ukiwa na kipengele cha miezi 12 zaidi.

Huyu ni mchezaji wa pili kusajiliwa na Tottenham kipindi hiki baada ya Victor Wanyama aliyesajiliwa toka  Southampton.

Anaingia katika kikosi cha Spur kushindana na Harry Kane katika nafasi ya ushambuliaji na hii inaifanya Tottenham kuwa na washambuliaji wawili ambao walikua bora zaidi msimu uliopita.

Janssen alimaliza msimu uliopita katika ligi kuu ya Uholanzi akiwa mfungaji bora akifunga magoli 26 katika michezo 34 akifunga pia goli 1 katika michezo 6.


No comments

Powered by Blogger.