AZAM TV YAMWAGA BILIONI 23 KUONYESHA LIGI KUU TANZANIA BARA

Azam TV leo imeweka historia mpya katika soka la Tanzania baada ya kusaini mkataba mpya wa udhamini kwaajili ya haki ya matangazo ya ligi hiyo kuweza kurusha moja kwa moja michezo ya ligi kuu Tanzania bara wenye gharama ya shilingi bilioni 23.


Azam imeingia katika mkataba huu mpya wa miaka mitano baada ya ule wa awali kumalizika ambapo kila timu ilikua Mkataba inapata Shilingi milioni 100 kwa msimu lakini kwa mkataba huu mpya kila klabu itaingiza karibu mara mbili ya pesa hizo.

Katika mkataba uliosainiwa leo kila klabu itapata Shilingi milioni 42 kwa mafungu matatu ambayo ni Shilingi ilingilingi kwa msimu na fungu la mwisho la milioni 42 litatolewa kwa mfumo tofauti na ilivyo sasa.

Pengine mkataba huu mpya utapunguza zile hisia za timu kupanga matokeo kwani Timu inayoshika nafasi ya juu katika msimamo inafaidika kwa kupata zaidi na itakwenda hivyo hadi chini.

Hii ina maana kwamba ligi itakapoisha, timu zitazokuwa juu kimsimamo zitapata fedha nyingi zaidi na zilizo chini zitaendelea kusota kwa kupata kiduchu.

Lengo kuu la kuleta mfumo huu ni  kuhakikisha kuwa ushindani unakuwepo na kila kikosi kuona umuhimu wa kukaa juu katika msimamo wa ligi hali itakayochangia ushindani uwanjani kwa kila timu kutaka kushinda karibu kila mechi ili mwisho wa ligi ifaidike.


No comments

Powered by Blogger.