SIMBA YAIKANDAMIZA POLISI MOROGORO BAO 6-0.

Wekundu wa Msimbazi Simba ambao wako katika kambi ya mazoezi mjini Morogoro jioni hii wameikandamiza Polisi Morogoro bao 6-0.


Mchezo huo wa kirafiki uliopigwa jioni hii mjini Morogoro ni wa majaribio kwa kocha mpya Joseph Omog ambaye amejichimbia na kikosi chake katika milima ya Uluguru kujiandaa na msimu mpya.

Mshambuliaji raia wa Ivory Coast Fredrick Blagnon na Ibrahim Ajib walifunga bao 2 kila mmoja huku Chipukizi Mohammed Kijiko na Abdi Banda wakifunga bao moja kila mmoja kukamilisha ushindi mkubwa kwa Simba.

KIKOSI CHA SIMBA 

Vicent Agban, Janver Bokungu, Mohamed Hussein Shabalala, Novat Lufunga, Mwanjal, Mohamed Ibrahim/Said Ndemla, Jamal Mnyate/Daniel Lyanga, Mzamil Yasin,Fedrik, Ibrahim Ajib, Shiza Kichuya

No comments

Powered by Blogger.