DAAAH! YANGA YAPIGWA TENA SAFARI HII NA WAGHANA

Mabingwa wa Tanzania bara Yanga wamezidi kupotea katika mbio zao za kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika baada ya kuchabangwa bao 3-1 na Medeama ya Ghana.


Mpaka mapumziko tayari Yanga walishapigwa bao hizo 3-1 Mohammed Abas akifunga bao mbili huku Daniel Aboa akifunga bao 1 wakati bao la kufutia machozi la Yanga likifungwa na Simon Msuva.

Yanga imebaki na pointi yake moja katika kundi A wakiwa wamebakiza mechi mbili ile ya nyumbani dhidi ya Mo Bejaia na ile ya ugenini dhidi ya TP Mazembe ya Congo.

No comments

Powered by Blogger.