SHEVCHENKO KOCHA MPYA TIMU YA TAIFA YA UKRAINE

Chama cha soka nchini Ukraine kimemteua mshambuliaji wa zamani wa AC Milan na Chelsea Andriy Shevchenko kuwa kocha mkuu mpya wa timu ya tamku ya nchi hiyo.


Shevchenko mwenye miaka 39, aliyechezea timu ya taifa mara 111, atajaza nafasi ya Mykhaylo Fomenko, aliyeondoka baada ya taifa hilo kuondolewa katika michuano ya Euro 2016 katika hatua ya makundi.

Shevchenko alikuwa msaidizi wa Fomenko Ukraine waliposhindwa mechi zao zote dhidi ya Ujerumani, Ireland Kaskazini na Poland.

Mchezaji huyo wa zamani wa Dynamo Kyiv, aliyestaafu mwaka 2012, hajawahi kuhudumu kama kocha mkuu katika maisha yake.


No comments

Powered by Blogger.