YANGA YATAWALA TUZO ZA WASHINDI WA MSIMU ULIOPITA TANZANIA

Mabingwa wa Tanzania bara Yanga SC wameendelea kutawala katika tuzo za washindi wa msimu uliopita wa ligi kuu ya soka Tanzania bara.


Baada ya Msimu wa 2014/2015 Simon Msuva kuibuka kidedea akitwaa zawadi ya mchezaji bora msimu uliopita ni zamu ya Juma Abdul baada ya kutangazwa kwamba ndiye mchezaji bora kabisa kwa msimu uliopita akiwashinda Mohammed Hussein wa Simba na Kichuya wa Mtibwa Sugar.

Ukiacha tuzo ya mchezaji bora Yanga pia imekua ndiyo bingwa wa msimu uliopita ikitoa pia mfungaji bora Amiss Tambwe, Mchezaji bora wa kigeni ambaye ni Thaban Kamusoko na kocha Bora Hans De Pluijm.

Simba wao kwa upande wao wametoa wachezaji wawili waliopata tuzo Ibrahim Ajib Mgomba aliyeshinda tuzo ya goli bora na Mohammed Husein ambaye alikua mchezaji bora chipukizi.

Mtibwa Sugar ndiyo timu iliyojinyakulia tuzo ya timu bora yenye nidhamu.

WASHINDI WA TUZO HIZO KWA KIFUPI

   ● Washindi - Yanga
   ● Washindi wa pili - Azam FC
   ● Washindi wa Tatu - Simba SC
   ● Mfungaji bora - Amiss Tambwe
   ● Timu Yenye Nidhamu - Mtibwa Sugar
   ● Mwamuzi Bora - Ngole Mwangole
   ● Kocha Bora - Hans De Pluijm (Yanga)  
   ● Bora - Aishi Salum Manula (Azam FC)
   ● Goli bora - Ibrahim Ajib (Simba vs Mgambo)
  ● Mchezaji bora wa kigeni - Thaban Kamusoko (Yanga)
  ● Mchezaji bora Chipukizi - Mohammed Hussein "Tshabalala" (Simba)
   ● Mchezaji Bora wa ligi -Juma Abdul (Yanga SC)





~ www.wapendasoka.com

No comments

Powered by Blogger.