BAADA YA KUSAJILIWA CHELSEA KANTE ADAI NDOTO YAKE IMETIMIA

Kiungo mpya wa Chelsea Ng'olo Kante amesema kujiunga kwake kuichezea klabu hiyo ya London ni kutimia kwa ndoto yake ya kucheza katika klabu kubwa.



Kante mmoja kati ya wachezaji bora wa Leicester City ambao ni mabingwa wa Msimu uliopita katika ligi kuu ya England amesajiliwa na Chelsea toka Leicester City.

Kiasi cha paundi milioni 30 kimetumika kumsajili Kante kutoka Leicester City kwa mkataba wa miaka mitano. Leicester walimsajili mchezaji huyo kwa paundi milioni 6 na kuichezea klabu hiyo mara 40 akifunga bao moja tu.





No comments

Powered by Blogger.