SAMATA KUWEKA REKODI MPYA LEO KATIKA MICHUANO YA EUROPA LEAGUE

Nahodha wa Taifa Stars na mshambuliaji wa klabu ya Genk ya nchini Ubelgiji Mbwana Ally Samata leo ataweka historia mpya kwake na Tanzania.

Akiwa na klabu yake ya Genk Mbwana Samata atakua Mtanzania wa kwanza kucheza katika michuano ya Europa league inayoendelea leo usiku barani Ulaya.

Genk itatupa karata yake ya kwanza leo ikiwa nyumbani itakapopambana na klabu ya Budućnost ya Montenegro katika hatua ya pili ya michuano hiyo.

Mechi ya marudiano itapigwa ugenini wiki ijayo hivyo basi Genk wanatakiwa kushinda mechi hii kujiweka vyema kwaajili ya kutinga hatua ya tatu.


No comments

Powered by Blogger.