BARCELONA YAWEKA WAZI JEZI ZAO MPYA ZA UGENINI BILA NEMBO YA MDHAMINI

Mabingwa wa soka nchini Spain klabu ya Barcelona imeweka wazi jezi zake mpya za ugenini kwaajili ya msimu ujao.


Jezi hizo zilizowekwa katika mtandao wa klabu hiyo zikiwa katika picha zimevaliwa na wachezaji nyotpichatimu hiyo hazina nembo yoyote ya mdhamini baada ya kumalizika mkataba wa Quatar Airways waliokua wakiidhamini.

Mpaka sasa hakuna kampuni iliyoweza kufikia dau la paundi milioni 55.6 kwa msimu ambalo Barca wanataka kwa kampuni yoyote inayohitaji kuwadhamini.

Barca wataanza maandalizi ya msimu mpya kwa kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Celtic Mwishoni mwa mwezi huu.



No comments

Powered by Blogger.