TANZANIA YAPANDA NAFASI 13, ARGENTINA NAMBA 1 KATIKA UBORA WA SOKA DUNIANI.

FIFA Imetoa viwango vya ubora wa nchi wanachama wake kwa mwezi wa 6 ambapo Tanzania imepanda kwa nafasi 13 katika viwango hivyo.




Tanzania imepanda toka nafasi ya 136 mpaka nafasi ya 123 huku Kenya wakitia fora kwa kupanda mpaka nafasi ya 86 katika viwango hivyo vilivyotoka muda mchache uliopita ikipanda kwa nafasi 43.

Ureno ambao ni mabingwa wapya wa Euro 2016 wao wamepanda mpaka nafasi ya 6 wakati Chile ambao ni mabingwa waCopa America wanakamata nafasi ya 5 huku Argentina wakiendelea kukamata uongozi kwa kukamata nafasi ya kwanza katika Chati hiyo ikifuatiwa na Ubelgiji.

Kwa upande wa Afrika Algeria imeendelea kushika usukani kwa kuwa ya kwanza katika bara la Afrika huku ikishika nafasi ya 32 katika ubora duniani.

Mataifa ya mwisho kabisa katika orodha hiyo ya FIFA ni mataifa ya kanda ya Afrika Mashariki yaani Djibouti, Eritrea na Somalia ambazo zote zinaorodheshwa katika nafasi ya 205.

Kumi bora barani Afrika

  1. Algeria (32)
  2. Ivory Coast (35)
  3. Ghana (36)
  4. Senegal (41)
  5. Misri (43)
  6. Tunisia (45)
  7. Cameroon (53)
  8. Morocco (54)
  9. DR Congo(59)
  10. Mali (61)

Kumi bora duniani

  1. Argentina
  2. Ubeljiji
  3. Colombia
  4. Ujerumani
  5. Chile
  6. Ureno
  7. Ufaransa
  8. Spain
  9. Brazil
  10. Italia



No comments

Powered by Blogger.