SAMATA AJIHAKIKISHIA NAMBA KATIKA KIKOSI CHA GENK WAKIPATA USHINDI MUHIMU KATIKA EUROPA LEAGUE

Nyota ya nahodha wa Tanzania Mbwana Ally Samatta imeendelea kung'ara baada ya kujihakikishia namba katika kikosi cha Genk kinachoshiriki michuano ya Europa League hivi sasa.


Genk imebuka na ushindi wa bao 1-0 katika uwanja wake wa nyumbani wa Cristal baada ya kuwaadhibu Cork City ya Ireland katika hatua ya tatu ya mechi za mtoano ya michuano ya Europa League.

Goli pekee la Genk lilifungwa na Leon Bailey dakika ya 31 ya mchezo goli likilodumu mpaka mwisho wa mchezo.

Sasa Genk wako hatua moja kabla ya kuingia hatua ya makundi na watatakiwa kulinda ushindi wao katika mechi ya marudiano wiki ijayo huko Ireland.

1 comment:

  1. Point of correction; Cork City ni ya Ireland na sio Scotland.

    ReplyDelete

Powered by Blogger.