Mmmh AZAM HAYA MAZOEZI SASA SIFA, YAINYUKA KOMBAINI YA ZANZIBAR BAO 1-0

Mabingwa wa kombe la Kagame Azam FC wanaendelea na maandalizi yao ya msimu mpya wa ligi kuu Tanzania bara pamoja na mashindano mbalimbali mjini Zanzibar.


Azam FC ambayo inanolewa na makocha wapya toka Hispania iko mjini Zanzibar kwa takribani wiki moja sasa wakijiandaa na msimu mpya wakiweka kambi katika hoteli ya Mtoni Marine.

Azam wameonekana wakifanya mazoezi ya ufukweni muda mwingi lakini kwa siku ya jana wachezaji walifanya mazoezi ya kujenga stamina katika bwawa la kuogelea mazoezi yaliyoongozwa na kocha wa viungo Porges Pablo.

Wakati huo huo Azam jana Usiku waliweza kuifunga timu ya Kombaini ya Mjini Zanzibar kwa bao 1-0 mchezo huo ulipigwa katika dimba la Amani mjini humo.







No comments

Powered by Blogger.