KUMBE IBRAHIMOVIC ALIMTOSA BECKHAM NA KUJIUNGA NA MAN UNITED

Zlatan Ibrahimovic amesema alikataa kujiunga na klabu ya Marekani ya FC MIAMI inayomilikiwa na gwiji wa zamani wa Manchester United David Beckham ili kujiunga na  Manchester United.



Ibrahimovic ambaye ameshawahi kucheza na David Beckham katika klabu ya PSG nchini Ufaransa amejiunga na Manchester United katika dirisha hili la usajili kama mchezaji huru kwa mkataba wa mwaka mmoja.

David Beckham alikua na mazungumzo na mkali huyo wa kuzifumania nyavu ili akajiunge na Miam FC lakini Ibra aligoma fursa hiyo na kuamua kujiunga na United

No comments

Powered by Blogger.