MAMBO YAZIDI KUWA MAGUMU KWA RONALDINHO GAUCHO,ACHEZA MECHI YA KIRAFIKI KUPATA PESA

Kama kuna mtu anatamani maisha yangerudi nyuma ili aende akarekebishe alipokosea basi Ronaldinho Gaucho angekua mmoja wa watu hao.
 Tangu mwaka 2015 alipotemwa na klabu ya Atletico Mineiro Ronaldinho hajapata timu ya kuichezea swala ambalo ni gumu kuliamini kwa wale wanaomfahamu mchezaji huyo na kipaji alichonacho katika soka la kimataifa.

Kazi ya Ronaldinho ni soka hivyo anaposhindwa kupata timu ya kuchezea inakua ngumu kukabiliana na maisha akiwa kama mchezaji maarufu na katika kuhakikisha anakua na fedha za kujikimu wakati huu anapotafuta timu ya kuichezea.

Juzi Jumapili akiwa nchini Guatemala Ronaldinho alicheza katika mechi ya kirafiki ili kupata pesa wakati timu zenye upinzani wa jadi nchini humo za Municipal na Comunicaciones zilipopambana huku Ronaldinho akicheza katika timu zote mbili moja kila kipindi

Mchezo huo ulimalizika kwa sare ya 2-2 huku Ronaldinho akishindwa kufunga wala kutoa mchango katika magoli yote.

Akiwa na miaka 36 hivi sasa Ronaldinho amefunga magoli manne tu ndani ya miaka miwili iliyopita hii inaonyesha kabisa kiwango chake kinaelekea "Jioni".



2 comments:

  1. life sometimes liko fasta sana

    ReplyDelete
  2. Thanks for picking out the time to discuss this, I feel great about it and love studying more on this topic. It is extremely helpful for me. Thanks for such a valuable help again. estancia tours from buenos aires

    ReplyDelete

Powered by Blogger.