IBRAHIMOVIC APIGA BONGE LA GOLI, MAN UNITED IKIPIGA BAO 5

Mshambuliaji mpya wa Manchester United Zlatan Ibrahimovic ameanza kazi rasmi ndani ya kikosi hicho baada ya kufunga bao moja katika ushindi wa bao 5-2 waliupata dhidi ya Galatasaray.



Ibrahimovic alifunga bao la kwanza kwa "tik tak" akiunganisha mpira wa Antonio Valencia dakika ya 3 tu ya mchezo lakini Galatasaray waliamka na kusawazisha bao hilo kwa goli la Sinan Gümüs akiunganisha mpira wa faulo uliopigwa na Wesley Sneidjer.

Mpaka mapumziko Tayari United walishakua nyuma kwa bao 2-1 lakini kipindi cha pili Mourinho alibadilisha wachezaji watano ambao waliubadilisha mchezo na kufanikiwa kupata magoli manne.

Nahodha Wayne Rooney alifunga bao 2,Juan Mata akafunga bao 1 na Fellaini akafunga bao moja katika mchezo huo uliopigwa katika dimba la Ullevi huko Sweden.

Man United itakua dimbani tena Jumatano wiki hii kucheza na Everton katika dimba la Old Trafford ikiwa ni mechi ya mwisho ya maandalizi kabla ya kuikabili Leicester City Jumapili katika mechi ya ngao ya Hisani.

No comments

Powered by Blogger.