EVERTON YAKATAA DAU LA CHELSEA KUMSAJILI LUKAKU

Everton wamekataa ofa ya paundi milioni 57 iliyotolewa na Chelsea kutaka kumsajili mshambuliaji Romelu Lukaku.


Lukaku ambaye alisajiliwa na Everton akitokea Chelsea ameonyesha nia yake ya kutaka kurudi katika klabu hiyo ambayo inanolewa na Mutaliano Antonio Conte.

Everton wanaamini kwamba mshambuliaji huyo Raia wa Ubelgiji thamani yake ni kubwa zaidi na wameweka kipengele cha kununuliwa kwa paundi milioni 75 na kuwataka Chelsea waongeze pesa.


No comments

Powered by Blogger.