ZABALETA KUMFATA MANCIN INTER MILAN

Klabu ya Inter Milan iko katika mazungumzo na  Manchester City kutaka kumsajili beki wake wa pembeni Raia wa Argentina Pablo Zabaleta.

 Wawakilishi wa Beki huyo mkongwe walikua mjini Milan Jumanne kukamilisha dili la kumtoa beki huyo katika kikosi cha Manchester City ambacho kitakua chini ya Kocha Pep Guadiola.

Dili hilo likikamilika litamuunganisha mchezaji huyo na kocha wake wa zamani anayeifundisha Inter Milan hivi sasa  Roberto Mancini kukiwa pia na uvumi wa kutakiwa na AS Roma.

No comments

Powered by Blogger.