RONALDO AIVUSHA URENO AKIWEKA REKODI MPYA,ITALIA YACHAPWA, UBELGIJI YAPETA
Mechi za mwisho za hatua ya makundi katika michuano ya Euro zilimalizika jana kwa mechi nne kuchezwa katika viwanja vinne nchini Ufaransa.
Cristiano Ronaldo akiiongoza Ureno jana walifanikiwa kuambulia sare ya bao 3-3 na vinara Hungary katika mchezo ambao Ronaldo alifunga bao 2 na kusaidia kupatikana bao la kwanza lililofungwa na Luis Nani.
Dunia ilishuhudia Cristiano Ronaldo akiinusuru timu yake mara tatu kila Hungary walipofunga Ronaldo alisawazisha mpaka mpira kuisha kwa sare hiyo ya bao 3-3 sare ambayo imeifanya Ureno kukamata nafasi ya tatu kwa kufikisha pointi 3 na inasonga mbele kwa kuwa best looser timu ya 3 ambayo haijafungwa mchezo wowote.
Kwa magoli hayo aloyofunga Ronaldo jana ameweka rekodi nyingine kwa kuwa mchezaji wa kwanza kufunga katika fainali 4 za michuano ya Euro na amebakiza goli moja tu kuifikia rekodi ya Michel Platini ya goli 8.
Ameweka pia rekodi mpya ya kuwa mchezaji wa kwanza kucheza mechi 17 za michuano ya Euro akiwazidi Edwin van der Sar na Lilian Thuram waliocheza mechi 16.
Katika mechi nyingine ya kundi hilo la F katika michuano hiyo Iceland imetinga hatua ya 16 bora kwa kuifunga Austria kwa bao 2-1.
Mechi zingine hiyo jana zilikua mechi za kundi F ambapo Italia ilikubali kichapo cha bao 1-0 toka kwa Ireland huku Ubelgiji wakiibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Sweden na kuzifanya Ubelgiji,Italia na Ireland kusonga mbele.

No comments