UCHAGUZI STAND UNITED WAKARIBIA

Timu ya soka ya Stand united ya mkoani Shinyanga ipo katika mikakati ya kufanya uchaguzi wake wa viongozi wa kampuni hiyo.



Akithibitisha kuhusu hilo Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa timu
hiyo,Alexander Sanga amethibitisha kuwepo kwa uchaguzi huo.
"Ni kweli tutafanya uchaguzi kwa awamu mbili,katika awamu ya kwanza
Uchaguzi wetu utafanyika tarehe Juni 24 na uchaguzi huo utakuwa kwajili
Ya kuchagua wajumbe wawili kutoka kundi letu la wanahisa 42 kuingia
katika bodi ya wakurugenzi" alisema Sanga.

Sanga amesema katika uchaguzi wa awamu ya pili utakaofanyika tarehe 3 Julai utakuwa ni uchaguzi wa kumchagua Mwenyekiti na Kaimu mwenyekiti wa bodi ya Stand united.

Sanga amesema fomu za uchaguzi zimeanza kutolewa leo hii(Juni 17) na zinapatikana katika ofisi zao zilizopo pale Stendi ya zamani.
 Gharama za fomu ni shilingi 150,000/- kwa nafasi ya mwenyekiti,Kaimu mwenyekiti ni Shilingi 100,000/- na nafasi ya wajumbe ni shilingi 50,000/- tu.

Akielezea kuhusu usajili,Sanga amesema timu yao inaendlea na usajili na karibu wachezaji wote wamelewana nao.
" Kwa sasa timu yetu inapanga bajeti kwajili ya kambi na kisha tutampelekea mdhamini wetu Acacia na timu yetu itaingia kambi tarehe 28 June" alisema Sanga.
Sanga amesema pia timu yake hiyo ina mikakati ya kumtafuta kocha mkuu mpya.

IMETOLEWA NA
ALEXANDER SANGA
MKURUGENZI WA HABARI NA MAWASILIANO
STAND UNITED COMPANY LIMITED
0715052491

No comments

Powered by Blogger.