COPA AMERICA : MAREKANI YAITWANGA ECUADOR NA KUTANGULIA NUSU FAINALI (+Video)

Wenyeji wa fainali za Copa America Marekani wametinga hatua ya nusu fainali baada ya kuifunga Ecuador kwa bao 2-1 katika mchezo wa robo fainali uliopigwa usiku wa kuamkia leo.




Marekani ilitangulia kupata bao la kwanza likifungwa na Mchezaji wa zamani wa Tottenham Clint Dempsey dakika ya 22 ya mchezo bao lililodumu mpaka mapumziko.

Kipindi cha pili Gyas Zardes aliongeza bao la pili kabla ya  Ecuador kustuka na kupata bao la kufutia machozi dakika ya 74 likifungwa na Michael Arroyo katika mchezo ambao ulimalizika kwa timu zote kuwa pungufu baada ya wachezaji Antonio Valencia wa Ecuador na Jermaine Jones kutolewa kwa kadi nyekundu.

Highlights za mchezo huo


No comments

Powered by Blogger.