EURO 2016 : POLAND NA UJERUMANI HAKUNA MBABE, UKRAINE YATUPWA NJE YA MASHINDANO

Mabingwa wa dunia Ujerumani jana walilazimishwa sare ya bila kufungana na majirani zao Poland katika mchezo wa pili katika makundi ya michuano ya Euro 2016 nchini Ufaransa



Mechi hiyo ya Kundi C ilikua ya pili katika Kundi hilo Ikitanguliwa na ile ya awali baina ya Ireland kaskazini na Ukraine

Mechi hiyo ya awali ilimalizika kwa ushindi wa bao 2-0 ambao Ireland waliupata wakiwafunga Ukraine ambao wameonekana kuwa mdebwedo

Matokeo hayo yanalifanya Kundi hilo kuwa na timu tatu zinazoweza kutinga hatua ya robo fainali, Ujerumani na Poland wenye pointi 4 kila moja na Ireland kaskazini yenye pointi 3 huku Ukraine ikibaki bila pointi.

No comments

Powered by Blogger.