TAIFA STARS NI USHINDI TU LEO DHIDI YA MISRI

Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars leo itakua na shughuli moja tu ya kuifunga Misri katika mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za kombe la Mataifa ya Afrika mwakani.


Misri inayoongoza katika kundi G itaingia katika mchezo wa leo ikihitaji sare tu kuweza kuungana na mataifa mengine ambayo tayari yameshafuzu kwa fainali hizo za Gabon.

Stars itakua ikiwategemea nyota wake wote akiwemo nahodha Mbwana Samata na mshambuliaji toka TP Mazembe Thomas Ulimwengu ambao wamekua msaada mkubwa kwa timu hiyo siku za karibuni.

Stars inashika nafasi ya 3 katika kundi hilo ikiwa na pointi 1 tu wakati Misri wanaongoza na pointi zao 7 na ushindi pekee ndiyo silaha ya kuipa matumaini Stars leo.

STARS KWANZA TUSONGE MBELE

No comments

Powered by Blogger.