COPA AMERICA : WENYEJI USA WAAMBULIA KICHAPO MECHI YA UFUNGUZI

Michuano ya kombe la bara mataifa ya America imeanza usiku wa kuamkia leo kwa wenyeji timu ya Taifa ya Marekani USA kukubali kichapo cha bao 2-0 toka kwa Colombia.


Mchezo huo wa ufunguzi ulipigwa katika dimba la Levi katika mji wa Santa Clara ambapo kikosi cha Juggen Klinsman kilipewa nafasi kubwa ya kushinda mchezo huo wakiwa nyumbani na kiwango chao bora hivi sasa.

Mlinzi Cristian Zapata alitangulia kuipatia Colombia bao la kwanza kabla ya James Rodriguez hajafunga bao la pili kwa njia ya penati dakika chache kabla ya mapumziko.

Michuano hiyo itaingia katika siku yake ya pili usiku wa leo kwa mechi tatu Costa Rica ikicheza na Paraguay mchezo utakaoanza saa 6 usiku.
Haiti ikicheza na Peru saa 8 na nusu usiku na Brazil wakicheza na Ecuador saa 11 alfajiri kesho.


No comments

Powered by Blogger.