SHIKAMOO RONALDO : ATOA BONUS YOTE YA KUTWAA UBINGWA WA ULAYA KWA MASIKINI

CRISTIANO RONALDO ameendelea kuonyesha moyo wa huruma kwa wasiojiweza baada ya kuelekeza pesa zake zote za bonasi ya  kushinda ubingwa wa ligi ya mabingwa barani Ulaya ziende kusaidia wasiojiweza.


Kiasi cha pesa kinachokaribia kufikia paundi 500,000 ambazo Ronaldo alizipata baada ya kuisaidia Real Madrid kushinda ubingwa wa Ulaya amezielekeza zote kwa wasiojiweza.

Kabla ya mechi ya fainali dhidi ya Atletico Madrid Ronaldo alimwelekeza wakala wake Jorge Mendes kugawia wasiojiweza kiasi chochote kitakachopatikana katika fainali hiyo.

Ronaldo anamalizia mapumziko yake mjini Ibiza Spain kabla ya kuungana na wachezaji wenzake katika timu ya taifa ya Ureno kwaajili ya michuano ya Euro 2016 nchini Ufaransa.

No comments

Powered by Blogger.