BAADA YA KUKIPIGA MIAKA 21 NDANI YA NEWCASTLE STEVEN TAYLOR ASEMA SASA BASI

Ni nadra sana kwa mchezaji kudumu katika klabu moja kwa muda mrefu na hii inatokana na changamoto mbalimbali kama mchezaji.


Hali ni tofauti kwa Mlinzi wa Newcastle United Steven Taylor ambaye amedumu na klabu hiyo kwa miaka 21 na sasa ameamua kusema inatosha sasa na tayari ameamua kuangalia changamoto nyingine sehemu nyingine pindi mkataba wake itakapoisha mwishoni mwa mwezi huu.

Taylor mwenye miaka 30 ametumikia klabu hiyo kwa misimu 13 na kucheza michezo 268 huku mchezo wake wa mwisho ukiwa dhidi ya Tottenham ambapo Newcastle ilishinda bao 5-1.

Alijiunga  na Newcastle United mwaka 1995 lakini alisaini rasmi mkataba wa kucheza kama mchezaji wa kulipwa mwaka 2003

No comments

Powered by Blogger.