PSG YAICHOKOZA LIVERPOOL YAPANGA KUMSAJILI COUTINHO
Moja kati ya wachezaji wanaotajwa sana na mashabiki wa Liverpool ni Philipe Countinho Kiungo mshambuliaji raia wa Brazil.
Basi taarifa zilizoenea leo kuhusu mchezaji huyo bora mara mbili wa Liverpool ni mpango wa matajiri wa jiji la Paris PSG kutaka kumsajili mchezaji huyo.
Paris Saint-Germain (PSG) wamemweka Coutinho kama mmoja kati ya wachezaji walio katika mipango yao ila bado hawajapeleka ombi rasmi la kutaka kumsajili nyota huyo ambaye yuko Marekani hivi sasa na timu yake ya taifa katika michuano ya Copa America inayoanza usiku wa kuamkia leo.
Coutinho mwenye miaka 23 alisaini mkataba mpya wa miaka mitano mwaka jana wa kubaki Anfield na itakua ngumu kuona mchezaji huyo akiikataa PSG hasa kwa kuzingatia kwamba Liverpoool haitocheza katika ligi ya mabingwa msimu ujao.

No comments