SERENGETI BOYS YAJIPIGIA SHELI SHELI WADAU WARIDHIKA NA SOKA
Pambano kati ya Timu ya taifa ya vijana ya Tanzania chini ya miaka 17 Serengeti Boys na Sheli sheli chini ya miaka 17 limemalizika kwa Serengeti Boys kushinda kwa bao 3-0.
Nyota wa mchezo huo wa kuwania kufuzu kwa fainali za vijana za Afrika alikua ni beki wa pembeni wa Serengeti Nickson Kibabage ambaye alifunga bao la kwanza na kusababisha upatikanaji wa bao la tatu ambalo lilifungwa kwa njia ya penati na Ally Hussein.
Nickson alifunga bao la kwanza dakika ya 16 kisha Ibrahim Abdallah akafunga bao la pili dakika ya 22 huku bao la tatu likifungwa kipindi cha pili kwa penati na Ally Hussein.
Mchezo wa marudiano utafanyika nchini Sheli sheli ambapo bingwa wa jumla atakutana na timu ya Afrika Kusini kwa umri huo.
Wadau kadhaa waliokua uwanja wa Taifa waliridhishwa na kiwango kizuri kilichoonyeshwa na vijana hao ambao ni hazina kwa soka la badae

![]() |
| Huyu ndiye Nickson Kibabage |

No comments