COPA AMERICA : COLOMBIA YAINYUKA MAREKANI NA KUKAMATA NAFASI YA 3

Timu ya taifa ya Colombia imeibuka kama washindi wa tatu wa michuano ya Copa America Centenario 2016 nchini Marekani.



Colombia imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji Marekani goli pekee la mshambuliaji Carlos Bacca dakika ya 13 ya mchezo.

Michuano hiyo itafikia tamati usiku wa kuamkia kesho kwa saa za Afrika mashariki kuanzia saa 9 alfajiri kati ya Argentina na Mabingwa watetezi Chile.



No comments

Powered by Blogger.