URENO YATINGA ROBO FAINALI KISHUJAA, YAUNGANA NA POLAND NA WALES


Nahodha wa Ureno na mshambuliaji wa timu hiyo Cristiano Ronaldo amezidi kuonyesha umwamba wake baada ya kusaidia kwa kiwango kikubwa kupatikana bao pekee katika mechi ya hatua ya 16 bora dhidi ya Croatia.



Iliwabidi Ureno kusubiri mpaka dakika za lala salama katika muda wa nyongeza kupata bao hilo pekee baada ya mpira ulipigwa na Cristiano Ronaldo kutemwa na kipa Wa Croatia na kumkuta Ricardo Quaresma aliyeingia kama mchezaji wa akiba katika mechi hiyo.

Croatia itabidi wajilaumu wenyewe kwani wamekosa nafasi nyingi za wazi huku Ureno wakikosa kabisa nafasi muhimu za kufunga mpaka ilipopatikana nafasi hiyo iliyozaa goli huku Ukuta wa Ureno ukionekana imara zaidi ya mechi zilizopita Akianza mlinzi Wa kati Fonte ambaye alicheza pamoja na Pepe tofauti na mechi zilizopita ambapo Pepe alikua akicheza pamoja na Ricardo Carvalho.

Katika mechi zingine hiyo jana Poland iliibuka na ushindi dhidi ya Uswis wakishukuru changamoto ya mikwaju ya penati kuwavusha huku kiungo mpya wa Arsenal ya England Granit Xhaka akikosa penati na kuwapa Poland ushindi ambapo sasa watakutana na Ureno.

Gareth Bale akiiongoza Wales wameendelea kufanya vyema baad ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya ndugu zao Ireland Kaskazini.



No comments

Powered by Blogger.