MOURINHO KUMRUDISHA LUIS NANI MANCHESTER UNITED

Moja kati ya vyanzo vya habari nchini Uturuki vinaripoti leo kwamba kocha mpya wa Manchester United Jose Mourinho anataka kumrudisha winga wa zamani wa klabu hiyo Luis Nani klabuni hapo kwaajili ya msimu ujao.

Nani anayeichezea Fenerbahce ya Uturuki hivi sasa aliondoka Old Trafford msimu uliopita wakati kocha Luois Van Gaal alipoamua kumuuza yeye pamoja na Robin Van Perse.

Imeelezwa kwamba Nani anaweza kuondoka katika klabu hiyo kurudi England kama United wataweza kulipa paundi milioni 6.3 ambayo iko katika mkataba wake lakini United hawako tayari kulipa kiasi hicho cha pesa.

Nani ana miaka 29 hivi sasa na inasemekana yuko tayari kuhamia tena Old Trafford kama klabu hizo mbili zitakubaliana.

No comments

Powered by Blogger.