COPA AMERICA : BRAZIL YAIANGAMIZA TAHITI,ECUADOR NA PERU SARE

Kiungo mshambuliaji wa Liverpool Philip Countinho ameibuka shujaa wa timu yake ya taifa ya Brazil baada ya kuongoza maangamizi ya bao 7-1 wakiifunga Tahiti.


Mchezo huo wa raundi ya pili katika kundi B kwenye michuano ya Copa America inayoendelea nchini Marekani ulipigwa usiku wa kuamkia leo.

Philip Countinho alifunga hat-trick katika mchezo huo akifunga mabao hayo dakika ya 14,29 na dakika ya 90 huku Gabriel na Lucas Lima wakufunga bao moja kila mmoja huku Renato Augusto akifunga mabao mawili na James Marcelini akiifungia Tahiti bao la kufutia machozi.

Katika mchezo mwingine wa kundi hilo la B Ecuador walitoshana nguvu na Peru kwa kwenda sare ya bao 2-2 Enner Valencia na Milla Bolanos wakifunga mabao kwa upande wa Ecuador wakati Cueva na Flores wakifunga kwa upande wa Peru.

No comments

Powered by Blogger.