MOURINHO AANZA KAZI RASMI : AMSAJILI BEKI TOKA VILLAREAL

Kocha wa Manchester United Jose Mourinho amefanya usajili wake wa kwanza kwa kumsajili beki wa kimataifa wa Ivory Coast na klabu ya Villareal Eric Bertrand Bailly.

Bailly amesaini mkataba wa miaka minne kukiwa na kipengele cha kuongeza miaka miwili kuichezea Manchester United na sasa anatafutiwa kibali cha kufanya kazi nchini England 
Bailly, mwenye miaka 22 amecheza mechi  47 akiwa Villareal tangu alipojiunga na klabu hiyo mwezi Januari mwaka 2015.
Beki huyo Raia wa Ivory Coast ameichezea timu yake ya taifa mara 15 na ni mmoja kati ya wachezaji walioipa Ivory Coast Ubingwa wa kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2015 akicheza mechi zote katika mashindano hayo.

No comments

Powered by Blogger.