KUELEKEA MECHI KATI YA ITALIA NA UBELGIJI LEO: HUU NDIYO UCHAMBUZI YAKINIFU
Ukiniomba nikutajie mechi tano bora za hatua za makundi za Euro mechi ya kwanza kukutajia itakuwa kati ya Italia na Ubelgiji. Na ndiyo mechi ambayo nitakuletea uchambuzi leo hii.
UPI NI UBORA NA UDHAIFU WA ITALIA ?, NA KIPI KIKIFANYIKA WATASHINDA MECHI HII?.
Ukiitoa Romania ambayo kwenye mechi za hatua za kufuzu EURO iliruhusu magoli mawili tu kwenye mechi za makundi ya kufuzu EURO, Italia ni timu iliyofuatia kwa kuruhusu magoli machache ikiwa imeruhusu magoli matatu tu. Hapo ndipo ubora wa Italia unapoanzia. Buffon, Barzagli, Bonucci na Chiellini ni wachezaji pekee wenye uhakika wa kuanza leo kwenye kikosi cha Conte na ndio wanaojenga ubora wa Italia. Italia ni timu ambayo ina safu nzuri ya ulinzi kuliko Ubelgiji kwa hapo kesho.
Kwa mara ya kwanza tangia nianze kuiangalia Italia naishuhudia ikienda na safu butu ya ushambuliaji na usishangae kuona kwa mechi za hivi karibuni za timu ya Taifa kumuona Daniele De Rossi akiwa na uwiano mzuri wa kufunga kuliko mshambuliaji wao Pelle. Ingawa udhaifu wa Italia hauanzii kwenye Safu ya ushambuliaji lakini ni ukweli usiofichika kuwa ubutu wa safu ya ushambuliaji ni udhaifu mkubwa walionao. Timu ya ushindi ni ile inayojilinda vizuri na yenye mtu mwenye uwezo wa kukufungia goli wakati wowote, Ndiyo maana wakati Fulani Mourinho alipokuwa Italia alikuwa amejidhatiti vizuri kwenye kujilinda ila akilini mwake akiwa anajua Eto’o na Diego Milito walikuwa wanauwezo wa kumletea goli wakati wowote, vivyo hivyo na alipokuwa na ukuta mgumu wa Cahill na John Terry uliokuwa unazawadiwa na magoli ya Diego Costa.
Udhaifu wa Italia pia haujaishia kwenye ubutu wa safu ya ushambuliaji pekee. Majeruhi ya Marco Verrati, Claudio Marchisio yameleta pengo kubwa sana kwenye kikosi cha Conte. Kwanini nasema hivo? Kutokuwepo kwa Verrati na Marchisio kunamaanisha ya kuwa Conte atawatumia Thiago Motta, Daniele De Rossi na Florenzi kwa eneo la kati kwa mfumo wake pendwa wa 3-5-2. Hii inatafsiri gani? Ukimwangalia De Rossi, Motta na Florenzi Si viungo ambao wanaweza kutengeneza nafasi nyingi za kufunga, hivyo basi kwa mahitaji ya mfumo wa 3-5-2 itatakiwa De Rossi awe anarudi kumsaidia Thiago Motta kukaba, kupokonya mipira na kuanzisha mashambuliaji na awe anafika mpaka kwenye box la Ubelgiji akitokea kwenye box la timu yake, hivyo hii itadumaza sana ubunifu wa kutengeneza nafasi za kufunga, hivyo kuzidi kudumaza ubutu wa safu ya kushambulia. Au kwa kuwa ukiwa unatumia mfumo wa 3-5-2 viungo watatu wa kati hutakiwa kufanya kazi kwa pamoja, hivo pindi Italia itakapokuwa inashambuliwa viungo wote watatu watatakiwa kusaidiana kuzuia na kwa jinsi walivyo itakuwa ngumu kwao kutengeneza shambulizi za kushtukiza hivo kuzidi kuongeza ufinyu wa utengenezaji wa nafasi za magoli.
KIPI WAKIFANYE ITALIA WASHINDE MECHI HII?
Conte anatakiwa aendelee kuuamini mfumo wake wa 3-5-2 , tatizo linakuja kwenye uchaguzi wa wachezaji. Najua wachezaji wote waliochaguliwa wanaingia vizuri kwenye mfumo wa Conte, ila kwa kesho Conte anatakiwa aizuie safu bora ya ushambuliaji ya Ubelgiji kwa kushambulia, kwa kuwaweka pembeni viungo wenye asili ya kushambulia kama Candreva na El Shaarawy. Conte anatakiwa amsahau kwa leo Matteo Darmian kwa sababu kumwanzisha Darmian kutakuwa na maana ya kuwakaribisha Ubelgiji kushambulia, ndipo hapo watakuwa wamefanya kosa .
Kuwaruhusu Ubelgiji wakushambulie kwa safu yao ile ya ushambuliaji itawadharirisha. Njia pekee ya kuizua safu ya ushambuliaji ya Ubelgiji ni kuanzisha Viungo wenye asili ya kushambulia ili kuwafanya wazuie na kizuri zaidi Ubelgiji ana safu mbovu ya ulinzi hivyo Conte atakuwa na nafasi kubwa ya kuwatangulia kufunga na ukizingatia ana safu nzuri ya ulinzi, utafanya Ubelgiji kuwa watumwa wa mchezo na hapo ndipo umuhimu wa Matteo Darmian utahitajika kulinda ushindi.
Kitu kizuri kitakochomsaidia Conte ni kumwanzisha Eder ambaye ni yeye pekee anayeweza akatengeneza muunganiko mzuri wa safu ya ushambuliaji na yeyeto kati ya Pelle ambaye ndiye anafaa kuanza na Eder. Zaza,Immobile na Lorenzo wanatakiwa wawe watu watakaokuja kutimiza jukumu litakalowashinda Eder na Pelle.
UPI NI UBORA NA UDHAIFU WA UBELGIJI? KIPI WAKIFANYE WASHINDE.
Ukizungumzia shubiri ya mioyo ya mabeki lazima uwataje kina Yannick Carrasco, Dries Mertens, Michy Batshuayi, Origi, Lukaku, Benteke,De Bruyne na Hazard. Ni timu yenye safu kali ya ushambuliaji na huu ndio ubora wao. Safu iliyofunga goli 24 kwenye mechi za hatua za kufuzu EURO, na kizuri zaidi hakuna aliyejuu ya umri wa miaka 29.
Udhaifu wa Ubelgiji upo kwenye safu ya ulinzi tena udhaifu wao umeimarishwa na kutokuwepo kiongozi wao Vincent Kompany. Pengo la Kompany ni kubwa sana ikizingatia ni mchezaji kiongozi na ni mlinzi mzuri sana. Ubelgiji kwa mechi tano zilizopita wamekuwa wakitoka nyuma kwa kusawazisha na kushinda na pia hawajawahi kupata Clean sheet tangia September 6 mwaka jana. Hii ni mbaya sana hasa utakapokutana na timu yenye ulinzi mzuri kama Italia kwani ikikutangulia inakuwa ni shida kushinda kwa sababu ya ubora wa ulinzi wao.
KIPI WAKIFANYE UBELGIJI WASHINDE?
Fellaini ni mtu ambaye atahitajika sana kesho kwa Ubelgiji , Kwanini? Italia watakuwa na Thiago Motta, huyu mtu ndiye mwenye alama za siri za mwanzo ya mashambulizi ya Italia. Hivyo anahitajika mtu ambaye ataziba na kukaba njia zote za mipira ya hatari na sehemu inapotokea mipira hiyo ya hatari. Mtu huyo ni Fellaini ni mzuri sana kwa kuharibu mipango ya timu pindi anapopewa jukumu hilo.
Kwa leo Wilmots anatakiwa aangalie pembeni na kuwaanzisha kwa pamoja De Bruyne na Hazard wacheze nyuma ya mshambuliaji mmoja huku De Bruyne akitokea kulia mwa mshambuliaji wa mwisho huku Hazard atokee mgongoni mwa mshambuliaji wa mwisho, hii itawafanya wawe na uhakika wa kutengeneza nafasi nyingi za magoli na kufunga magoli mapema yatakayoziba udhaifu wafu.
MWISHO:
Timu itakayoziba udhaifu wake na kutumia ipasavyo ubora wake ndiyo itakayoshinda. Kizuri cha kusubiria ni kuona kama Conte alikuwa sahihi kumwacha Pirlo wakati akijua Verrati na Marchisio hatoenda nao Ufaransa. Kesho Motta atakuwa miongoni mwa wachezaji watakaong'ara kwa sababu atakuwa anataka kuwanyamazisha mashabiki wanaopinga yeye kupewa jezi namba 10.Kuanzia magolikipa mpaka mshambuliaji Ubelgiji wanatimu nzuri ni wakati wao huu, wanatakiwa kupigana.
Martin Kiyumbi ( 0657 77 10 77, 0744080891).
JUMATATU NJEMA NA MUNGU AKUBARIKI SANA.

No comments