COPA AMERICA : GOLI LA MKONO LAITUPA BRAZIL NJE YA MASHINDANO,ECUADOR YAPETA (+VIDEO HIGHLIGHTS)
Miamba ya soka duniani Brazil imeungana na Uruguay kuwa mataifa makubwa yaliyoaga mapema katika mashindano ya Copa America mwaka huu.
Brazil ilikubali kichapo cha bao 1-0 toka kwa Peru ambao sasa wamemaliza mechi za makundi wakiwa vinara wa kundi B wakiwa na pointi 7 wakifatiwa na Ecuador wenye pointi 5 huku Brazil wakiambulia pointi 4.
Wakati Peru wakiwafunga Brazil bao hilo 1-0 Ecuador wao waliwakandamiza Haiti kwa bao 4-0 mechi zote hizo zikipigwa mapema alfajiri ya leo.
Goli pekee lililoizamisha Brazil lilifungwa na Raul Ruidiaz goli ambalo limelalamikiwa kama mfungaji aliushika mpira kabla hajafunga na marudio ya picha za televisheni zinaonyesha kwamba ni kweli mfungaji aliusukumiza mpira kwa mkono golini. (Waweza kuangalia highlights za mchezo hapo chini)
Ecuador wao waliibuka na ushindi mwepesi toka kwa timu dhaifu ya Haiti magoli ya ndugu wawili Enner Valencia na Antonio Valencia na magoli mengine ya Jaime Ayovi na Christian Noboa.
HIGHLIGHTS
PERU 1-0 BRAZIL
ECUADOR 4-0 HAITI

No comments