KUELEKEA KATIKA MECHI YA WALES NA ENGLAND LEO HUU NDIYO UCHAMBUZI
Ni kati ya mechi za kuvutia ingawa inaweza ikawa siyo bora. Na huu ndiyo uchambuzi wangu kuelekea mechi hiyo.
UPI UBORA WA WALES?
Ubora wa Wales unaanzia jinsi wanavyojilinda, kwa haraka haraka waweza kufikiria wanamtindo wa kupaki gari lakini sivyo. Ukiangalia mechi iliyopita walitumia mfumo wa 5-4-1. Ambapo walikuwa na mabeki watatu wa kati, ambapo mmoja alicheza kwenye nusu ya eneo la katikati, hii iliifanya Wales kuwa na ukuta imara piakuanzisha mashambulizi kwa mipira mirefu ambayo wakati mwingine ilipokuwa inapotea ilikuwa inawakuta wachezaji wa Wales wakiwa eneo lao la kujilinda hivyo kuwa salama. Aina hii ya ulinzi ndiyo silaha kubwa kwa timu ya Wales.
Pia kitu kingine kinachowabeba Wales ni matokeo ya kwao ya mechi iliyopita ambayo walishinda hivyo watacheza kwa kutaka kushambulia wakati sahihi na siyo kila wakati.
KIPI WAKIFANYE WALES ILI WASHINDE?
Kwanza kabisa wanatakiwa waendelee kuuamini mfumo wao wa 5-4-1. Mfumo huu unampa nafasi kubwa Bale kwenye mashambulizi ya kushtukiza na ikizingatia ana kasi nzuri . Pia Wales wanatakiwa waendelea kuanzisha mashambulizi kwa mipira mirefu na waachane na utamaduni wa kuanzisha mashambulizi katikati kwani kwa mfumo wao na aina ya wachezaji walio nao wanakuwa hatari sana wanapoanzisha mashambulizi kwa mipira mirefu.
Faida ya kutokuanzia mashambulizi katikati ni kwamba ni ngumu kwa England kuingilia mchezo na mipango yao, ila mipira mirefu inawapa uhakika wa kutokuingiliwa kwenye mipango yao na wanakuwa na uhakika wa mambo mawili, kwanza kutokana na kasi ya Bale uhakika wa kufunga utakuwa mkubwa, pili wakati mipira itakapopotea kwa bahati mbaya wanakuwa na uhakika wa kujilinda, kwani wachezaji wengi watakuwa hawajahama maeneo yao .
Wales wana viungo wenye tabia ya kukaa uwanjani wakimwangalia kiungo mpinzani mwenye madhara kwao ambao ni David Edwards na Joe Allen. Wakati timu inaposhambulia Edwards huwa haangalii mchezo, badala yake huwa anatembea karibu na kiungo mwenye madhara na kuwa kwenye nafasi nzuri ya kuchukua mipira pindi timu inapopoteza. Pia Wales wanatakiwa waendelee kutokuchezesha mshambuliaji wa kati ili kuwafanya Ramsey, Bale na Jonny Williams kuwa wanaliacha wazi eneo hilo ili kuwafanya mabeki wa kati wa England wajisahau kwa kujiona hawana mzigo mkubwa wa kukaba na wao kuingia kwa kushtukiza pindi mabeki wanapojisahau. Mwisho Wales wanatakiwa watengeneze ukuta mgumu kama wa mechi iliyopita.
UPI UBORA WA ENGLAND?.
Kwa mara ya kwanza tangia 2000 England inaenda na washambuliaji waliofikisha magoli 20 kwenye ligi kila mmoja ambao ni Vardy na Kane. Siwezi nikasema ubora wa England unaanzia hapa ila ni sehemu ya hatari sana. Kiwango cha Harry Kane mechi iliyopita hakiwezi kikakufanya utoe imani kwake. Ubora wa England upo pembeni. Kyle Walker, Dany Rose, Raheem Sterling, Adam Lalana wana kasi sana ambayo inasaidia kusukuma mashambulizi na kama wakianza hii itawasaidia kuwazuia Gunter na Taylor kupanda mbele kwenda kusaidia kushambulia kama walivyofanya kwenye mechi dhidi ya Slovakia. Muda mwingi watakuwa makini kwenye kuzuia na siyo kushambulia hivyo kupunguza nafasi za kufunga kwa Wales.
KIPI WAKIFANYE ENGLAND WASHINDE?
Moja ya tatizo walilonalo England ni wachezaji wao wa kiungo cha kati kutokukaa na mipira. Hii huwanyima asilimia nyingi ya umilikaji wa mpira pia na nafasi za kutengeneza magoli. Hivyo kwa mechi hii wanatakiwa wamwanzishe Wilshere ambaye anaonekana kurejea vizuri kwani anauwezo wa kumiliki mpira na kuifanya timu iwe na mipira mingi katikati, hii itakuwa na madhara makubwa kwenye timu ya Wales kwani viungo wao watakuwa hawana uwezo wa kupata mipira mingi.
England kwa leo wanatakiwa kubadili mfumo kutoka 4-3-3 wa mechi iliyopita kwenda 4-4-2. Hii itawapa nafasi kubwa kuwaanzisha kwa pamoja Vardy na Kane. Ambao wote wanauwezo wa kufunga. Pia kwa kuwaanzisha Vardy na Kane kwa pamoja kutawafanya mabeki wa Wales wa kati ambao kutokana na Mfumo wao ni watatu (Kama wakitumia mfumo wa mechi iliyopita) kuwa makini sana kwenye kuwazuia na kukosa nafasi ya kwenda kushambulia. Sitegemei tena Kane kupiga kona kwenye mechi hii na jukumu kubwa atakalo kuwa nalo ni kufunga tu. Pia Walker na Rose wanatakiwa kuwa makini wanapoenda mbele kushambulia kwani hapa ndipo ilipo funguo ya matokeo mabaya kwao kwani pindi watakapochelewa kurudi nyuma kulinda na kwa mtindo wa Wales kuanzisha mashambulizi ya kushtukiza kwa mipira mirefu itakuwa faida kwa Bale kuwaadabisha.
England wanatakiwa wasiendelee kuumizwa na matokeo dhidi ya Russia ingawa hii inaweza silaha yao kubwa kupata matokeo au kupoteza matokeo.
AHSANTENI NA MUNGU AWABARIKI.
Martin kiyumbi (0657 77 10 77, 0744 0808 91).
Facebook na Instagram : Martin Kiyumbi.

No comments