EURO 2016: UEFA KUIONDOA RUSSIA KATIKA MASHINDANO IKIWA..........

Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA Limeipa onyo la mwisho timu ya Taifa ya Russia kufuatia fujo zilizoletwa na mashabiki wao wakati wakicheza dhidi ya England siku ya Jumamosi.


Katika mechi hiyo iliyomalizika kwa sare ya bao 1-1 kulizuka fujo jukwaani na nje ya uwanja zilizosababishwa na mashabiki wa Russia na England katika mji wa Marseille.

Russia imeelezwa kuwa fujo zozote zitakazoletwa tena na mashabiki wao itapelekea kuondolewa katika michuano hiyo huku chama cha soka cha Russia (RFU) Kikilimwa faini kutokana na matumizi ya mafataki na ubaguzi wa rangi. Japokua onyo hilo ni kwa fujo zitakazotokea ndani ya uwanja pekee na wamepewa nafasi ya kukata rufaa.

Pamoja na onyo hilo Russia watatakiwa kulipa kiasi cha paundi 119,000 kutokana na fujo hizo.

Russia watacheza dhidi ya Slovakia siku ya Kesho jijini Lille Ufaransa na Wales Jumatatu Ijayo katika mji wa Toulouse.





No comments

Powered by Blogger.