BEKI WA ZAMANI WA MANCHESTER UNITED ATANGAZWA KUIFUNDISHA READING MSIMU UJAO

Klabu ya Reading inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini England (Championship) imemtangaza beki wa zamani wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Uholanzi Jaap Stam kama kocha wao mpya.
Staam mwenye miaka 43 ambaye aliichezea Uholanzi mambaye anachukua nafasi iliyoachwa wazi na McDermott aloyetimuliwa.

Stam ni mmoja kati ya wachezaji walioipa Manchester United makombe matatu msimu wa mwaka 1998/1999 akiitumikia klabu hiyo kwa misimu mitatu na sasa atajiunga na Reading kwa mkataba wa miaka miwili.

Jaap Stam aliyefahamika kwa uimara wake akicheza kama Beki wa kati akiichezea United aliwahi kuzichezea pia Lazio,AC Milan na Ajax.


Anakua kocha wa kwanza wa Reading ambaye hana asili ya Uingereza kuifundisha klabu hiyo  na atasaidiana na Waholanzi wenzake Andries Ulderink na Said Bakkana.

No comments

Powered by Blogger.